ChademaChadema

Chadema Walia na Hujuma Zinazofanywa Dhidi yao, Waitisha Kikao cha Dharura

Chama Cha Demokrasia na maendeleo Chadema kimeitisha Kikao cha dharura cha Viongozi wakuu wa Chama hicho, kitakachokuwa na lengo la kutathmini hali ya kisiasa ya Chama hicho kikuu cha Upinzani nchini Tanzania na kile walichokiita kama “ukandamizaji” na Njama za kukidhohofisha Chama hicho.

Chadema kupitia kwa Mkurugenzi wake wa mawasiliano na uenezi Brenda Rupia katika taarifa yake waliyoituma JamboTv, wametoa wito kwa wanachama na wafuasi wa Chama hicho pamoja na watanzania wote wanaoamini katika haki, kuwa tayari muda wowote kupokea maelekezo kutoka kwa Uongozi wa Chadema, wakisisitiza kutorudi nyuma katika kudai Tanzania yenye mfumo wa haki, uhuru na utawala wa sheria.

Hatua ya Chadema kutoa tamko hili inafuatia maamuzi ya Mahakama ya Tanzania leo Jumanne Juni 10, 2025 kutoa amri ya kusitisha kwa muda wa siku 14 shughuli za kisiasa za Chadema kutokana na kesi iliyokuwa imewasilishwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Zanzibar kwa takribani miaka 15 Bw. Said Mohammed pamoja na wenzake wawili waliokuwa Wajumbe wa bodi ya udhamini wakilalamikia upendeleo na kukosekana kwa usawa wa matumizi ya rasilimali za Chama hicho kwa pande mbili za Muungano wa Tanzania.

“Jaji ametoa hukumu hiyo bila chama kuwa na mawakili wake baada ya wakili wetu Jebra Kambole kujitoa kutokana na kuhisi kutotendewa haki. Jebra aliomba kesi kusitishwa hadi Chama kitakapopata wakili mwingine lakini Jaji alikataa na kuendela kusikiliza kesi kwa upande mmoja tu na kutoa uamuzi wake. Kwa mtazamo wetu uamuzi huu unachochewa zaidi na shinikizo la kisiasa badala ya msingi wa kisheria au haki huku imizi gatiwa hali ya kisiasa ilivyo nchini mwetu” imenukuliwa taarifa ya Brenda Rupia, Mkurugenzi wa Mawasiliano na uenezi Chadema.

“Ni dhahiri kuwa kuna njama za makusudi za kuingilia, kuchafua na kuvuruga uongozi halali wa Chadema kwa lengo la kuua operesheni yetu ya No Reforms, No election- harakati za kidemokrasia zinazodai mazingira huru na haki ya uchaguzi.”

Pia tumekuwa mashuhuda wa kilele cha siasa za vurugu na hujuma dhidi ya mikutano yetu ya hadhara jwa maelekezo ya wazi kutoka kwa baadhi ya Viongozi wa CCM. Polisi wamekuwa wakilazimisha kubadili viwanja vya mikutano, wakurugenzi

ALSO READ | Mwanaume wa Miaka 50 Afariki Akifanya Mapenzi na Mke wa Mtu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *