Augustine OkejepherAugustine Okejepher

Simba Wafanya Maamuzi Magumu, Augustine Okejepher Kupewa Thank You

Kiungo mkabaji wa Club ya Simba Augustine Okejepher hatokuwa sehemu ya Kikosi cha Simba msimu ujao mara baada ya uongozi wa Timu hiyo kufanya maamuzi magumu ya kuachana naye kwa kushindwa kuonyesha kiwango Bora kama walivyotarajia kabla ya kumsajili kutua klabuni hapo.

MAHITAJI ya Kocha Fadlu Davids kwa sasa ni makubwa MNO huku akitambua msimu ujao anashiriki ligi ya Mabingwa Barani Africa mashindano ambayo ni magumu sana ambayo timu nyingi Bora na zenye wachezaji wazuri wenye quality kubwa zinashiriki.

Kocha Fadlu anahitaji Kuifikisha Simba kwenye hatua za juu zaidi kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Barani Africa msimu ujao huku matumaini yakiwa ni makubwa ya kufanya vizuri kutokana na historia ya Simba iliyonayo kwenye mashindano hayo.

Kocha FADLU DAVID’S amewasilisha hitaji la kiungo mkabaji wa kigeni kwenye ripoti yake mezani kwa Tajiri mchezaji ambaye atakuja kuchukua nafasi ya Mnigeria Augustine Okejepher.

All the best man once lion always lion

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *