Mtoto wa Museveni Atoa Mpya “Baba Akistaafu Urais, Rais Ajae ni Mimi”

Jenerali Muhoozi Kainerugaba
Meseven vs Jenerali Muhoozi Kainerugaba

Mtoto wa Museveni Atoa Mpya “Baba Akistaafu Urais, Rais Ajae ni Mimi”

Mkuu wa Majeshi ya Uganda ambaye pia ni Mtoto wa Rais Yoweri Museveni, Jenerali Muhoozi Kainerugaba ametangaza nia yake ya kugombea Urais wa Uganda mwaka 2031, akisisitiza kuwa hakuna atakayemzuia kufikia azma hiyo baada ya Baba yake kuondoka madarakani.

Muhoozi ametoa kauli hiyo leo Jumanne, Novemba 17, 2026, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X, akieleza kuwa anajipanga kuwania Urais kwa muhula wa mwaka 2031 hadi 2036, huku mjadala kuhusu mrithi wa Rais Museveni ukiendelea ndani ya Chama tawala cha National Resistance Movement (NRM).

Tamko hilo limekuja siku chache baada ya Shirika la Habari la AFP kuripoti kuwa baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu ya Utendaji ya NRM (CEC) walipinga pendekezo la Muhoozi kuwa mrithi wa Museveni katika kikao cha Novemba 10, 2026, wakieleza wasiwasi kuhusu uzoefu wake katika uongozi wa kiraia na kauli zake kwenye mitandao ya kijamii.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa NRM, Richard Todwong, alikanusha taarifa hizo akisema kikao hicho kilijadili masuala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi, huku akisisitiza kuwa maamuzi rasmi ya Chama yatatangazwa kupitia njia zake za mawasiliano.

Hadi sasa Rais Museveni mwenye umri wa miaka 82 hajatangaza rasmi mrithi wake, huku baadhi ya Viongozi waandamizi wa NRM wakipendekeza aendelee kuwania Urais mwaka 2031.

Related Posts