Edo Kumwembe: Nilimsifia Chasambi ila Nimeangukia Pua
Nilijigamba sana mwanzoni mwa msimu kwamba huenda Ladaki Chasambi na Edwin Balua wangekuwa moto katika safu ya ushambuliaji ya Simba. Kumbe nilikuwa najidanganya tu, Napenda wachezaji wazawa wanapofanikiwa katika timu zetu Nilikuwa najidanganya tu
Kwa Chasambi niliona namna amavyokokota mpira kwa ustadi. Kwa Balua nilipenda pia jambo hilo lakini pia mashuti yake na namna anavyoweza kukata mipira yake katika faulo na kona. Kabla sijawaona nilikuwa nasimuliwa na waandishi wenzangu namna vijana hao mmoja kutoka Prisons mwingine kutoka Mtibwa Sugar walivyokuwa bora.
Ukisikia simulizi ulikuwa unapata picha kwamba Simba walikuwa wamenasa mawe mawili ya madini kama ambayo Mzee Laizer aliyanasa kule Arusha. Hata hivyo, kwa sasa yanaonekana sio madini tena na muda wowote ule wanaweza kutolewa kwa mkopo kwenda kwingineko. Hakuna ambaye atashangaa kama Simba wakichukua hatua hiyo.
Niliamini wangefuata nyayo za Clement Mzize aliyepasua katika kundi la washambuliaji wazuri wageni pale Yanga kisha akawa tegemeo klabuni. Katika mpira wetu hizi timu kubwa maeneo ya ulinzi na kiungo wazawa wamepambana kupata nafasi. Kule mbele baada ya kuondoka kwa John Bocco inaonekana Clement Mzize amerithi makali hayo japo kwa ujumla wake hajafukia mambo ambayo Bocco amefanya.
Hawa vijana wangu Chasambi na Balua kwa namna nilivyowaona mwanzoni mwa msimu niliamini wana kitu. Kitu ambacho kingelisaidia taifa katika siku za usoni. Kadri siku zilivyokwenda mbele ndivyo walivyoanza kupotea uwanjani. Walichoniangusha zaidi ni kwamba walishindwa kupata nafasi za kudumu katika Simba hii ambayo awali ilionekana kama inasuasua katika eneo la ushambuliaji.
Ndiyo, Leonel Ateba hajaeleweka mpaka leo miongoni mwa washambuliaji wa Simba. Joshua Mutale amekuja kueleweka mwishoni zaidi. Kama Chasambi alishindwa kuipora nafasi ya Mutale wakati ule atawezaje kuipora leo? Kibu Dennis hajawa na msimu mzuri, lakini bado Fadlu Davis anaona bora ampange Kibu kuliko Balua au Chasambi. Nini kimewatokea vijana hawa?
Watu wangu wa ndani wa Simba wananiambia vijana wetu ndio tatizo. Mmoja kati ya hao amewahi kufeli mara nne vipimo vya pombe vinavyoandaliwa ghafla na kocha Fadlu
ALSO READ | Edo Kumwembe: Pyramids Wametuonesha Mpira ni Pesa…..
Alikataa kuolewa ili amkomboe mama yake... Lakini mama ndiye aliyemuuza!
GORYANAH –Hii ni story ya Moto Sana yenye hisia na Mafunzo, binti jasiri anayepambana na siri nzito, umaskini na hatari kubwa kwa ndoto zake! Pakua app yetu ufurahie Sehemu ya 1 Hadi ya 5,na mwendelezo wake kila JUMAMOSI SAA MOJA KAMILI JIONI BURE!
Ukiona ujumbe wa allow notification bonyeza allow ili uwe mwanafamilia.