
EXCLUSIVE: Mustakabali wa Selemani Mwalimu Ndani ya Simba SC
Kocha mkuu wa Simba SC, Steve Barker, amemtaja mshambuliaji Selemani Mwalimu kama mmoja wa wachezaji nguzo anaotaka kubaki nao kwa ajili ya msimu ujao wa 2026/27. Hata hivyo, dili hili lina milima kadhaa ya kuvuka:
-
Changamoto ya Mkataba: Mkataba wa sasa wa mkopo wa Mwalimu hauna kipengele cha kumnunua jumla au kuuongeza muda. Hii ina maana kuwa lazima arejee Wydad AC kwanza kabla ya mazungumzo mapya kuanza.
-
Msimamo wa Wydad AC: Miamba hao wa Morocco wako tayari kumwachia mchezaji huyo kwa mauzo ya jumla (permetnent transfer) na si kwa mkopo mwingine.
-
Kikwazo cha Dau: Bei inayotajwa na Wydad inatarajiwa kuwa kubwa, jambo linaloweza kuwa mtihani wa kifedha kwa Simba SC.
Uamuzi wa Mchezaji: Licha ya kupata ofa kutoka klabu mbalimbali, Selemani Mwalimu ameipa kipaumbele Simba SC na yuko tayari kusubiri hatima ya mazungumzo kati ya timu hizo mbili kabla ya kuangalia upepo kwingine.
