FIFA Kumlipa Refa Omar Artan Baada ya Kukosa Kombe la Dunia 2026

FIFA Kumlipa Refa Omar Artan Baada ya Kukosa Kombe la Dunia 2026
FIFA Kumlipa Refa Omar Artan Baada ya Kukosa Kombe la Dunia 2026

Shirikisho la soka Duniani, FIFA, limekubali kumlipa Mwamuzi wa Somalia, Omar Artan, fedha zote alizokuwa anatarajiwa kupata katika kombe la Dunia 2026, licha ya kushindwa kushiriki Mashindano hayo.

Artan alikosa nafasi ya kusimamia mechi baada ya kunyimwa ruhusa ya kuingia nchini Marekani, moja ya Mataifa mwenyeji wa Mashindano hayo.

Kwa mujibu wa taarifa, Waamuzi wa kombe la Dunia wanaweza kulipwa hadi Dola 100,000 za Marekani, kulingana na idadi ya mechi wanazosimamia katika mashindano hayo.

FIFA imesema hatua hiyo inalenga kumlipa Mwamuzi huyo haki zake, kutokana na kuwa alikuwa tayari ameteuliwa rasmi katika orodha ya Waamuzi wa Mashindano hayo.

Tukio hilo limezua mjadala katika ulimwengu wa michezo kuhusu changamoto za usafiri na vibali vya kuingia nchini Marekani ambavyo vimeathiri washiriki wa Mashindano hayo makubwa duniani.

Related Posts