Nafikiri Fiston Mayele na Stephane Aziz Ki ndio wachezaji ambao walibeba project ya Yanga kwenye miaka mitatu ya mwisho : Kipindi Mayele yupo Yanga timu yote ilikuwa mabegani kwake ( Kama hatofunga basi atatoa pasi ya goli )
Baada ya Fiston kuondoka , Aziz Ki ndio akawa “Top Man” kwa Wananchi 🔥 Yaani timu inacheza kwa kumzunguka yeye ( Kuanzia kutengeneza nafasi na kufunga magoli “G/A” ) .
Wachezaji wote wameondoka Yanga na kwenda kwenye Top teams Afrika : Fiston ameenda Pyramid na msimu huu anacheza fainali ya CAFCL then Aziz Ki ameenda Wydad ambao ni mabingwa mara tatu wa CAFCL .
Hapa Wananchi walifanya Scout nzuri sana 👍 Hela ambayo wamepokea kutoka kwa hawa nyota wawili ni zaidi ya pesa waliotoa kuwanunulia