Julius Malema Ahukumiwa Miaka Mitano Gerezani

Julius Malema Ahukumiwa Miaka Mitano Gerezani
Malema ahukumiwa miaka mitano gerezani

MAHAKAMA nchini Afrika Kusini leo imemhukumu kiongozi wa upinzani Julius Malema, kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la kufyatua risasi kwa kutumia bunduki ya kivita katika mkutano wa hadhara miaka minane iliyopita.

Mamia ya wafuasi waliovaa mavazi mekundu ya chama chake cha Economic Freedom Fighters (EFF) walijikusanya nje ya mahakama wakati hukumu hiyo ikitolewa, katika kesi iliyokuwa na mvutano mkubwa wa kisiasa.

Hakimu Twanet Olivier alisema Malema alivunja sheria za umiliki na matumizi ya silaha kwa makusudi, baada ya kufyatua risasi angani mwaka 2018 wakati wa maadhimisho ya chama chake cha EFF.

Related Posts