MSANII wa Bongo Fleva, Lulu Abbas maarufu kama Lulu Diva ameamua kufunguka kwa mara ya kwanza kuhusu video zake za utupu kusambaa mitandaoni na kuibua sintofahamu miongoni mwa mashabiki zake na watu wake wa karibu.
Akizungumza na moja ya chombo cha habari nchini, Lulu amesema Video hizo zimesambazwa na aliyekuwa mpenzi wake (jina ameliweka kapuni) akidai kuwa anataka kumkomesha mrembo huyo na kumharibia maisha yake.
“Alikuwa anafosi anamwambia…. kwa nini hauposti, mbona huweki vitu? I want Lulu to die, afe kabisa asiishi katika haya maisha. Sijui hata nilichomfanyia ni nini, kuachana kila mtu anaachana.
“Hakuna kitu kikubwa alichoknifanyia kwenye maisha yangu mpaka afikie hatua ya kusema anataka kuniharibia maisha, meseji hizo hapo mnaziona ambazo alikuwa ananiambia.
“Kama ninavyokwambia, nilikuwa naongea naye kimapenzi kama mpenzi wangu, ni mtu ambaye najiamini kuongea naye kwa sababu alinipenda, namuona ni mtu mzima, ana umri wa miaka 55, ametulia, kwa hiyo huwezi kufikiria kama anaweza kufanya vitu kama hivyo na mimi nilikuwa tayari kutulia.
“Kwa sasa hivi mimi nimetulia najiuguza, naangalia tu afya yangu, lakini pia kumuomba Mungu, ni jambo jema kumuomba Mungu kwa sababu najua nimemkosea kutokana na kitu nilichokifanya.
Lulu Diva amesema hajui video nyingine atazitoa lini kwani anazo nyingi
“Lakini kama mwanaume niliyekuwa naongea naye kama mpenzi wangu nilikuwa najiachia… Unatoka kuoga, unaongea naye, sijui hata hizo video anazo ngapi, leo atatoa ipi na nyingine ipi, kujiachia kila mtu anafanya hivyo, mimi sijajirekodi amenirekodi yeye.
“…. Nikawa nampetipeti ili asitoe hizo video lakini ameamua kuzitoa, yawezekana anazo nyingi zaidi ya hiyo moja iliyotoka kwa sababu nilikuwa naongea naye kimapenzi, kuna wakati natoka kuoga, sikumbuki na sijui anazo ngapi sababu ni muda umepita na nyakati tofauti.
“Kwa sasa sina cha kufanya, najiuguza tu, sina wa kumlilia wala wa kumlaumu zaidi ya kujilaumu mwenyewe. Imenifanya niwe na picha nyingine zaidi kwa wanaume,” amesema Lulu Diva.