
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimedai kuwa Msaidizi wa Mwenyekiti wa Chama Taifa, David Jumbe, alitekwa usiku wa kuamkia leo Mei 20, 2026 na watu wasiojulikana kabla ya kufanikiwa kuwatoroka watekaji hap akiwa bado amefungwa pingu mkononi.
Kupitia taarifa iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii ya chama hicho, CHADEMA imesema tukio hilo lilitokea jana usiku ambapo David Jumbe alichukuliwa kwa nguvu na watu hao waliokuwa wakitumia gari ambalo halikufahamika mara moja.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baadhi ya madereva wa bodaboda walilifuatilia gari hilo jambo lililodaiwa kuwapa presha watekaji na hatimaye David Jumbe kufanikiwa kutoroka.
“Jana usiku tarehe 20 Mei 2026, Msaidizi wa Mwenyekiti wa Chama Taifa David Jumbe alitekwa na baadae alifanikiwa kuwatoroka watekaji akiwa na pingu mkononi baada ya Bodaboda kufukuzia gari la watekaji. Ameumizwa sana.”__ imesema taarifa hiyo.
Hadi sasa, mamlaka za serikali na vyombo vya ulinzi na usalama bado hazijatoa taarifa rasmi kuhusu tukio hilo lililoripotiwa na CHADEMA kupitia mitandao yao ya kijamii.
NB: This image is for informational purposes only and does not promote or encourage violence.
