Msanii wa UGANDA Alalamika Diamond Kulipwa Mamilioni Show ya Uganda

Msanii wa Uganda, Allan Toniks, ameibua gumzo mitandaoni baada ya kueleza hasira zake kufuatia kupewa kiasi kidogo cha chini ya dola 1000 kwenye tamasha, huku staa wa Tanzania #DiamondPlatnumz akilipwa kiasi cha shilingi milioni 750 za Uganda (zaidi ya Tsh milioni 600) kwa kushiriki kampeni ya kuhamasisha kahawa nchini humo.

Kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter), Toniks aliandika kwa hasira akisema,

“Na wanakuja kunipa chini ya dola 1000, nikikataa wanasema najifanya. 750M UGX? Acheni ujinga.”

Kauli hiyo imezua mjadala mkali mtandaoni. Wapo wanaoona hatua ya kumleta Diamond ni ya maana kwa sababu anavutia macho ya kimataifa, lakini wengine wanasema ni kudhalilisha vipaji vya ndani, huku fedha hizo zikitajwa kuwa zingeweza kusaidia jamii au kuendeleza wasanii wa Uganda.

Wengine walikumbusha kuwa wakazi wa Kiteezi walihitaji milioni 200 za Uganda tu kuboresha maisha yao, lakini serikali ikalipa kiasi kikubwa kwa mgeni ambaye hana uhusiano wa moja kwa moja na kahawa.

Tukio hili limeibua maswali juu ya kipaumbele cha serikali, na umuhimu wa kuwekeza kwenye wasanii wa ndani, huku pia likiwapa changamoto wasanii wa Uganda kuboresha brand zao ili kupewa heshima wanayostahili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *