
Ameandika @el_mando_tz
Leo ngoja niwaibie kitu Wanangu, Unajua hawa watu mimi nilikuwa nawatazama mbali sana🤔
Navy Kenzo ndio duo inayofanya mchanganyiko wa Afropop, Bongo Flava, Dancehall na Afrobeat, kitu ambacho kimewafanya wasimame tofauti na vikundi vingine vya muziki Afrika Mashariki.
Wote tunajua Bongo Flava ya kawaida mara nyingi hujikita kwenye mapenzi, maisha ya kila siku, na hutumia midundo yenye Swahili vibe ila Navy Kenzo wanasukuma zaidi upande wa Afropop, Dancehall na Afro-fusion, wakitumia Kiswahili na Kiingereza.
Toka wanaanza muziki unawaona kabisa wao malengo yao sio kulenga local market pekee, wanafikiria soko la kimataifa kwa namna wanavyofanya muziki wao.
Kilichowapa nguvu ni muunganiko wao, Unajua kuna wasanii wachache sana Afrika wanaofanya vizuri kama couple-duo (mfano Navy Kenzo wakiwa male-female🤔
Kinachowavutia wengi ni kupata ladha mbili tofauti mfano Aika anaweka nguvu ya female power & vocals, Nahreel analeta rap, melody na production ya sauti nzito kidogo( Aika anavutia wanaume Nahrel anavutia Warembo kwa bezi yake😂
Na wote tu ajua Nahreel ni producer mkubwa kupitia The Industry Studios, Jamaa amezifanya Production zao ziwe ni za viwango vya kimataifa, zikilinganishwa na hits kutoka Nigeria au Caribbean.
Ukiangalia tu unaona kabisa ni watu Wanaojali sana quality ya video, brand image na stage performance, wakitaka mashabiki wawaone kama global stars, si wa Tanzania pekee.
Hawa watu walitakiwa wawe na Matuzo makubwa sana ya Kimataifa ingawa wameshawahu kushiriki Tuzo kubwa ila haitoshi kushiriki tu.
Kwa kifupi, Navy Kenzo si tu wasanii wa kutoa ngoma, bali ni strategic artists wanaojua wanataka kuonekana wapi miaka mingi ijayo:
Hawa walitakiwa wawe kwenye jukwaa moja na Burna Boy, Wizkid, Davido, Diamond na wengine, wakiwa na identity ya Kitanzania.
Kwa sasa naona kama Wameridhika sana 🤔 wanafanya muziki kwa kuamua, huenda ndio yalikuwa malengo yao.
Ila Ubora wa muziki wao umewafunika asilimia 90 ya wenzao hapa Bongo, Wanajua nini wanafanya, hawapekekwi na Trends.
Mimi naamini Siku nzuri kwao zinakuja kama wataendeleza Ubora huu.

