Prince Dube Atua Hardrock FC Baada ya Kuondoka Yanga SC

Prince Dube Atua Hardrock FC Baada ya Kuondoka Yanga SC
Prince Dube Atua Hardrock FC Baada ya Kuondoka Yanga SC

Prince Dube Atua Hardrock FC Baada ya Kuondoka Yanga SC

Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga SC, Prince Dube, amepata changamoto mpya baada ya kukamilisha rasmi uhamisho wake kwenda klabu ya Hardrock FC ya nchini kwao, Zimbabwe, kwa mkataba wa miaka miwili.

Mshambuliaji huyo hatari anajiunga na klabu hiyo kama mchezaji huru kufuatia kumalizika kwa mkataba wake wa kuitumikia miamba ya soka la Tanzania, Yanga SC, ambapo alikuwa muhimili mkubwa kwenye safu ya ushambuliaji kabla ya kufunganya virago na kurejea nyumbani.

Hardrock FC, ambayo ni miongoni mwa timu zilizopanda daraja msimu huu kuelekea Ligi Kuu ya Zimbabwe, inatajwa kuwa na mikakati thabiti ya ushindani. Klabu hiyo inakuja kwa kasi ikiwa na mipango mikubwa ya maendeleo, ikiwemo uwekezaji kwenye miundombinu ya kisasa na ujenzi wa uwanja wao binafsi.

“Dube amesajiliwa rasmi na ameanza safari yake mpya ya soka katika ardhi ya nyumbani,” ilieleza taarifa rasmi kutoka Hardrock FC.

Uamuzi huu unahitimisha rasmi ukurasa wa Prince Dube katika Ligi Kuu ya NBC nchini Tanzania, huku akirejea kwenye ligi ya nyumbani kwao Zimbabwe akiwa na matumaini ya kuandika historia nyingine mpya na matajiri hao wapya wa soka.

Related Posts