Rais wa zamani wa Marekani Joe Biden amegunduliwa kuwa na “aina kali” ya saratani ya tezi dume, kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi yake binafsi siku ya Jumapili, na saratani hiyo imesambaa hadi kwenye mifupa.
“Rais Mstaafu Joe Biden alifanyiwa uchunguzi kwa uvimbe mpya kwenye tezi dume baada ya kupata dalili za kuongezeka kwa matatizo ya mkojo. Ijumaa iliyopita, aligunduliwa kuwa na saratani ya tezi dume, ikiwa na alama ya Gleason ya 9 (Kundi la Daraja la 5) na saratani hiyo imesambaa hadi kwenye mifupa,” taarifa hiyo kutoka ofisi yake ilisema.
Taarifa hiyo iliendelea kusema, “Ingawa hii ni aina kali zaidi ya ugonjwa huo, saratani inaonekana kuwa nyeti kwa homoni, jambo linalowezesha kudhibitiwa kwa ufanisi.”