
Rasmi: Yanga SC Yamsajili Peter Shalulile kutoka Mamelodi Sundowns
Mabingwa wa soka nchini, Yanga SC, wameendelea kuonyesha umakini wao kuelekea msimu mpya baada ya kumtambulisha rasmi mshambuliaji wa kimataifa wa Namibia, Peter Shalulile (32), kama mchezaji wao mpya.
Shalulile anajiunga na Wananchi kama mchezaji huru kufuatia kumalizika kwa mkataba wake na miamba ya Afrika Kusini, Mamelodi Sundowns.
Usajili huu mkubwa umetikisa sekta ya soka nchini na kuibua hisia kutoka kwa wadau mbalimbali. Miongoni mwao ni Mbunge wa Jimbo la Makete na shabiki wa Simba SC, Festo Sanga, aliyetania kupitia mitandao ya kijamii kwa kuandika: “Jirani mbona upo serious sana! Hutaki kabisa tubebe kombe? Shalulile mtu!”
Ujio wa mshambuliaji huyo unatajwa kuwa miongoni mwa usajili wa kishindo zaidi utakaotikisa na kuongeza hamasa katika Ligi Kuu ya NBC pamoja na michuano ya kimataifa
