Gerson Msigwa Gerson Msigwa

Serikali “No Reforms, No Election ya Mtandaoni ni Upuuzi”

Akizungumza na Mwananchi Communications Ltd kuhusu wimbi kubwa la watumiaji wa Mitandao ya Kijamii ‘ku-comment’ No reforms, No Election, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema “Watu wajiepushe na kampeni zisizokuwa na tija, watumie Mitandao kama fursa ya kujifunza Teknolojia mpya, wanapaswa kutambua na kujua kutumia Mitandao vibaya ni kupoteza Rasilimali Fedha kwa kuwa wanatumia bando”

Katika maelezo yake Msigwa amesema “Kinachoendelea kwenye Mitandao ni upuuzi. Huu ni upuuzi unaoendelea, Watanzania wajielekeze kujenga Nchi yao. Huwezi kuendesha Kampeni ya kuzuia Uchaguzi wakati Nchi imejiwekea kalenda yake.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *