Rais Samia Aunda Tume ya Uchunguzi wa Kijinai Ghasia za Uchaguzi Mkuu 2025

Rais Samia Aunda Tume ya Uchunguzi wa Kijinai Ghasia za Uchaguzi Mkuu 2025
Rais Samia Aunda Tume ya Uchunguzi wa Kijinai Ghasia za Uchaguzi Mkuu 2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameunda Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya Ghasia ya Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 ambapo amemteua Mhe. Shabani Ally Lila, Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Kamishna na Mwenyekiti wa Tume hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya leo Mei 18, 2026 iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses M. Kusiluka, Rais Samia pia amewateua majaji watatu wastaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuwa Makamishna wa Tume hiyo ambao ni Mhe. Gad John Mjemmas, Mhe. Awadh Mohamed Bawazir na Mhe. Aishieli Nelson Sumari.

Rais Samia amefanya uteuzi huo kwa kuzingatia mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Tume za Uchunguzi, Sura ya 32 katika kutekeleza mapendekezo ya Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani Yaliyotokea Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025.

Related Posts