Asubuhi ya leo ilipangwa kufanyika pre match conference, lakini katika mazingira yasiyo ya kawaida Simba SC hawajatokea eneo la tukio maana yake hawajafanya mahojiano na vyombo vya habari kuelekea Mechi ya kesho.
Chanzo changu kinaniambia Simba hawatambui kwa nini mechi ya tarehe 15 iliahirishwa …. Hivyo haitambui tarehe ya mechi ya kesho
Kuelekea mchezo wa Dabi ya Kariakoo dhidi ya Simba na Yanga unaotarajiwa kupigwa kesho majira ya saa 11:00 jioni kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, benchi la ufundi la timu ya Simba limegoma kuzungumza na waandishi wa Habari katika mkutano uliokuwa umefanyika makao makuu ya Benki ya Taifa ya Biashara (NBC).
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa benchi la ufundi la Yanga na wanahabari Ofisa Habari wa Bodi ya Ligi (TPLB) Karim Boimanda alisema wamefanya jitihada ya kuwatafuta viongozi wa Simba isipokuwa hawakuweza kupatikana.
“Simba walitakiwa kuwa hapa baada ya Yanga kumaliza mkutano wao na wanahabari tumefanya jitihada ya kuwatafuta kwenye siku ili watuambie wamepata changamoto gani tumeshindwa kuwapata hewani, alisema Boimanda.
Ofisa Habari huyo alisema taarifa zitaendelea kutolewa kupitia kurasa zao za mitandao ya jamii endapo kama Simba watatoa sababu iliyowafanya wasitokee.
Alisema kuhusu waamuzi ambao waliwatangaza hapo jana kutoka nchini Misri hawana wasi wasi nao kwa kuwa ni miongoni mwa waamuzi wenye viwango vya Kimataifa.
Awali mchezo huo ulipangwa uchezwe Machi 8, mwaka huu isipokuwa uliahirishwa kutokana na sababu ambazo mpaka sasa hazijafahamika.
Alikataa kuolewa ili amkomboe mama yake... Lakini mama ndiye aliyemuuza!
GORYANAH –Hii ni story ya Moto Sana yenye hisia na Mafunzo, binti jasiri anayepambana na siri nzito, umaskini na hatari kubwa kwa ndoto zake! Pakua app yetu ufurahie Sehemu ya 1 Hadi ya 5,na mwendelezo wake kila JUMAMOSI SAA MOJA KAMILI JIONI BURE!
Ukiona ujumbe wa allow notification bonyeza allow ili uwe mwanafamilia.