Tanzania Yapewa Pointi 3 Dhidi ya Congo Kufuzu Kombe la Dunia
Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limeipa Tanzania alama tatu dhidi ya Congo Brazzaville kufuatia kuondolewa kwa adhabu ya kufungiwa kwa Timu hiyo ya Taifa ya Congo Brazzaville ikiwa ni baada ya mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 kati ya Mataifa hayo iliyopangwa kuchezwa mwezi Machi 2024 kushindwa kufanyika kutokana na upande wa Congo kuwa umefungiwa.
Kufuatia uamuzi huu Taifa Stars sasa imefikisha alama 9, ikiendelea kushikilia nafasi ya pili kwenye kundi E nyuma ya Morocco yenye alma 15 huku Zambia ikishika nafasi ya tatu ikiwa na alama 6 na kufuatiwa na Niger, Congo Brazzavile pamoja na Eritrea.
Hata hivyo Timu ya kwanza pekee katika kundi ndiyo itakayofuzu moja kwa mojaKombe la Dunia 2026 ingawaje Tanzania ikiwa itamaliza nafasi ya pili bado inaweza kupata nafasi ya kucheza mtoano wa CAF (CAF Playoff) iwapo itakuwa miongoni mwa timu 4 bora za pili kutoka makundi yote 9 barani Afrika ambapo Mshindi wa mtoano huo atakwenda kwenye intercontinental playoff, ambako atapambana na Timu kutoka Mabara mengine kutafuta tiketi ya mwisho ya kufuzu.