Tathimini Yangu Kuhusu Maamuzi Mabovu ya Refa Hery Sasii Uwanjani….Tathimini Yangu Kuhusu Maamuzi Mabovu ya Refa Hery Sasii Uwanjani….

Tathimini Yangu Kuhusu Maamuzi Mabovu ya Refa Hery Sasii Uwanjani….

Tukio la Che Malone kumkwatua Tchakei- Ni Foul yeye akameza filimbi.

Tukio la Malone kumkwatua Sowah – Ni Foul yeye akameza filimbi.

Tukio la Chamoue kumuangusha Sowah – Ni Foul, ilifaa iwe penalti na Redcard ila yeye akapeta.

Kevin Nashon alionywa mara 2 baada ya kuwa na kadi ya njano – Ilifaa foul yake kwa Ngoma iwe second Yellow alafu aoneshwe Redcard lakini Sasii akapeta.

Tukio la Che Malone kumvuta na kumuangusha Sowah – Ni Foul ndani ya box ilifaa iwe penati na Redcard lakini Sasii alipeta.

Tukio la Ngoma kumvuta Serge Pokou – Ni Foul iliyokuwa Tactical na Ngoma alistahili Yellow Card lakini Sasii akapeta.

Tukio la Hamza kumvuta Elvis Rupia kwenye Box ni foul, Mwamuzi akapeta. Foul za kwenye box sio lazima mtu atoke damu. Unajiuliza Mwamuzi hakutaka Simba ifungwe au alitakaje?

Yapo matukio mengine aliamua kwa Favour ya Simba lakini Mwamuzi Msaidizi namba 2 (Hamdani Said anafanya semina kuelekea CHAN) alikuwa na maamuzi sahihi mnoo tena yupo serious na kazi yake hakuwa anaamua kumpa faida yeyote.

Ndiyo maana ananolewa kwenda CHAN 2025.

Mwamuzi Sasii alishawahi kufungiwa miezi 3 kwa kushindwa kuumudu mchezo kwa kushindwa kutafsiri sheria 17 za soka miaka kadhaa iliyopita, Leo amerudia. Kama TPLB isipompa adhabu yeyote watakuwa wanabariki matendo haya.

Simba SC walikuwa wanamlalamikia Mwamuzi Dahane Beida kwamba amewaua wakakosa Kombe, ila leo ukiwauliza Sasii amewapa faida wao wanajibu UBAYA UBWELA…..

Kachero!

CHAMBUA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *