Uongozi wa Mbeya City umeanza hesabu za kuiwinda saini ya winga wa Yanga, Farid Mussa ili kuongeza nguvu ya timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, ikiwa ni katika harakati za kukisuka kikosi hicho ili kilete ushindani zaidi.

Taarifa kutoka ndani ya timu hiyo , Farid ni miongoni mwa wachezaji wanaowindwa na kikosi hicho kitakachoshiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao, kwa lengo la kukiboresha kwa kushirikiana na nyota wengine watakaojiunga nao.

“Ni kweli Farid yupo katika mipango ya Mbeya City na kama kila kitu kitaenda sawa basi tunaweza kukamilisha uhamisho huo mapema iwezekanavyo, ni mchezaji mzuri na mwenye uzoefu tunayeamini atatusaidia huko mbele,” kilisema chanzo chetu.

Kwa upande wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mbeya City (CEO), Ally Nnunduma alisema tayari mipango ya kukisuka kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao imeanza, ingawa ni mapema sana kuweka wazi ni mchezaji gani wanayemuhitaji ili kuongeza nguvu zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *