Tetesi za soka Ulaya Jumapili: Man United wapata mbadala wa nahodha Bruno FernandesTetesi za soka Ulaya Jumapili: Man United wapata mbadala wa nahodha Bruno Fernandes

Tetesi za soka Ulaya Jumapili: Man United wapata mbadala wa nahodha Bruno Fernandes

Manchester United wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Ureno na Sporting Pedro Goncalves, 26, kama mbadala wa kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes, 30, ikiwa atahamia Saudi Arabia msimu huu. (Jumapili Mirror), nje

Bayern Munich wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza na Crystal Palace Eberechi Eze, 26, baada ya mafanikio ya msimu wa kwanza wa kiungo wa kati wa Ufaransa Michael Olise akiwa na klabu hiyo ya Ujerumani. (Football Insider), nje

Crystal Palace ingependa Eze atie saini mkataba mpya nao licha ya vilabu vingine vya Ligi Kuu ya Uingereza Arsenal, Tottenham na Manchester City kumtaka. (I)


Winga wa Liverpool Mholanzi Cody Gakpo, 26, na winga wa Brighton Mjapani mwenye umri wa miaka 28 Kaoru Mitoma pia wako kwenye orodha ya wachezaji wanaolengwa na Bayern Munich. (Christian Falk)

Mshambulizi wa Brazil Rodrygo, 24, ameiambia Real Madrid kwamba anataka kusalia katika klabu hiyo licha ya vilabu mbalimbali vya Ligi ya Premia kumtaka. (Marca – In Spanish}

Manchester City itawasilisha ombi la kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Lyon na Ufaransa chini ya umri wa miaka 21 Rayan Cherki, 21, wiki hii. (Fabrizio Romano)


Arsenal wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa mabingwa wa Italia Napoli kwa mshambuliaji wa Sporting na Uswidi Viktor Gyokeres, 26. (Star on Sunday)

Mustakabali wa Ange Postecoglou kama mkufunzi wa Tottenham unatarajiwa kuamuliwa wiki ijayo huku nafasi ya Muaustralia huyo mwenye umri wa miaka 59 ikiwa katika hatari kubwa licha ya kushinda Ligi ya Europa. (Sunday Telegraph)

Kiungo wa kati wa Uhispania Rodri atapewa kandarasi mpya na Manchester City, huku klabu hiyo ikitamani kutambua hadhi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kama mmoja wa wachezaji bora zaidi duniani. (Sunday Mirror)


Barcelona itafuatilia nia yao ya kumnunua fowadi wa Manchester United na Muingereza Marcus Rashford, 27, ikiwa dili la winga wa Liverpool mwenye umri wa miaka 28 kutoka Colombia Luis Diaz litashindwa kutekelezwa. (Mundo Deportivo – In Spanish)

Huenda Newcastle ikalazimika kumlipa kipa wa England na Burnley James Trafford, 22, huku meneja Scott Parker akitaka kuwahifadhi wachezaji wake bora kufuatia kupandishwa kwao katika Ligi ya Premia. (Football Insider)

Tottenham wanatafakari iwapo watafanya uhamisho wa mkopo wa Mfaransa Mathys Tel mwenye umri wa miaka 20 kutoka Bayern Munich kuwa wa kudumu. (Sky Sports),


Arsenal haitajaribu kumnunua Raheem Sterling kutoka Chelsea baada ya winga huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 30 kuwa na kipindi kigumu cha mkopo akiwa na The Gunners. (Express)

Bosi wa Fulham Marco Silva ndiye mgombea anayeongoza kuwa kocha mkuu mpya wa Juventus ya Italia huku mkurugenzi wa michezo anayekuja Damien Comolli shabiki wa Mreno huyo mwenye umri wa miaka 47. (Sky Italia – In Itali)

Mshambulizi wa zamani wa Liverpool Dirk Kuyt, 44, ni miongoni mwa wale wanaotajwa kuwa msaidizi mpya wa mkufunzi wa Reds Arne Slot huko Anfield. (Liverpool Echo)

BBC

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *