Hadi Huruma Man United Chali, Tottenham Mabingwa Europa Ligi 2025
Tottenham Hotspur imekomesha ukame wa makombe wa miaka 17 baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya Europa 2025 kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Manchester United katika dimba la San Mames, Bilbao Uhispania.
Kipigo hicho kimeikosesha Manchester United nafasi ya kushiriki michuano ya Ulaya msimu ujao huku kocha wa Spurs, Ange Postecoglou akidumisha rekodi yake ya kutwaa kombe kwenye msimu wake wa pili kwenye kila klabu aliyowahi kuinoa.
FT: Tottenham 🏴 1-0 🏴 Man United
⚽ 42’ Johnson.