
Msanii nyota wa muziki wa injili Upendo Nkone amepokea zawadi ya gari kutoka kwa mashabiki wake, katika hafla maalum iliyofanyika Aprili 23, 2026 ndani ya Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Gari hilo limenunuliwa kupitia michango ya mashabiki wake walioungana kwa lengo la kuthamini mchango wake mkubwa katika muziki wa injili na kugusa maisha ya watu wengi kupitia nyimbo zake zenye ujumbe wa kiroho.
Mchakato mzima wa ukusanyaji wa michango hiyo ulisimamiwa na Resty Bulla pamoja na Lillian Mwasha, ambao walihakikisha zoezi hilo linafanikiwa kwa uwazi na ushirikiano mkubwa kutoka kwa wadau mbalimbali.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na mashabiki, wadau wa muziki wa injili pamoja na watu mbalimbali waliokuja kushuhudia tukio hilo muhimu. Tukio hili linaendelea kuonyesha nguvu ya mshikamano kati ya wasanii na mashabiki wao, hasa katika kukuza na kuendeleza sanaa ya muziki wa injili nchini.
Kwa habari zaidi na matukio mengine kama haya, endelea kufuatilia taarifa zetu kila siku.
