Waliokua wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) na kundi la G55 ambao walijiengua kutoka Chadema hivi karibuni, wamejiunga na chama cha Ukombozi wa Umma(CHAUMMA) na kukabidhiwa kadi zao za Chama.
Wakati huohuo Kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho wajumbe wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho wamejaza nafasi za uongozi zilizokua wazi ikiwemo Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu.
Katika nafasi hizo zilizokuwa Wazi tayari zimejazwa na Salum Mwalimu amekua Katibu Mkuu Taifa, Devotha Minja amekaimu nafasi ya Makamu mwenyekiti Bara na Benson Kigaila amekaimu nafasi ya Naibu katibu Mkuu bara.