Sakata la Chadema na Msajili, Makala Asema “Asitafutwe Mchawi”
Katika kile kinachoonekana kuikingia kifua Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini kuhusiana na sintofahamu inayoendelea baina ya ofisi hiyo na CHADEMA, Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa CPA Amos Makalla amesema mzizi wa ‘sintofahamu’ hiyo umesababishwa na CHADEMA wenyewe kutokana mmoja wao kukimbilia ‘kushtaki’ kwa ‘Msajili’
Akizungumza kwenye siku yake ya kwanza mkoani Kagera, katika ziara ya siku saba kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa, CPA Makalla amedai kuwa ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini kuna mgogoro mkubwa wa wenyewe kwa wenyewe hali inayopelekea kuwa na makundi kinzani miongoni mwao
Akizungumzia kampeni ya ‘No Reforms, No Election’ inayoendeshwa na CHADEMA ikilenga ‘kuzuia’ uchaguzi endapo mabadiliko ya msingi ya mifumo ya uchaguzi wanayodai isipotafutiwa majawabu, CPA Makalla amedai kuwa hicho ni ‘kivuli’ cha kususia uchaguzi kwakuwa chama hicho hakikujiandaa