Wanajeshi 200 Wauwawa Burkina Faso
Kundi moja la wanamgambo huko Afrika Magharibi lililo na mafungamano na kundi la al-Qaeda, limesema limewauwa wanajeshi 200 wa Burkina Faso katika kambi moja ya kijeshi wiki hii.
Haya ni kwa mujibu wa kundi moja linalofuatilia harakati za mitandaoni za wanamgambo wa kiislamu.
Hapo jana, kundi la Jama’a Nusrat ul-islam wa al-Muslimin, JNIM, lilisema kwamba limewauwa wanajeshi 60 ila leo hii limeongeza idadi hiyo.
Shirika la habari la Reuters halikuweza kuthibitisha taarifa ya kundi hilo nayo serikali ya Burkina Faso haikujibu ombi la shirika hilo la habari la kutoa tamko kuhusiana na madai hayo.
Ingawa hakujatolewa taarifa rasmi na serikali, wakaazi watatu wa mji wa kaskazini wa Djibo uliovamiwa, wameliambia shirika la habari la Reuters kuwa dazeni kadhaa za wanajeshi na raia wameuwawa.
Tangu kufanyika kwa tukio hilo, kundi la JNIM limefunga njia ya kuelekea katika kambi ya kijeshi ya Djibo