Wanaume Mwanza Wamelalamika Kunyimwa Unyumba na Wake zao
Na Anania Kajuni, Mwanza.
Baadhi ya wanaume jijini Mwanza wamelalamika kunyimwa unyumba na wake zao huku ugumu wa maisha ukitajwa kuwa sababu.
Wakizungumza na Jambo TV wakiwa kwenye ligi ya mpira wa miguu iliyoanzishwa na Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) Wilaya ya Nyamagana wamesema wanakosa haki hiyo kwa sababu ya uchumi wao kuwa duni.
“Ukatili ambao tumekuwa tukikutana nao majumbani ni pamoja na kunyimwa unyumba ni sehemu ya ukatili mkubwa sana katika maisha ya binadamu hasa kwa wanaume tunakutana nao sana hasa pale unapokuwa na uchumi duni shida inakuwa kubwa ila ukiwa na uchumi unaweza kusikilizwa kwa haraka lakini tumekosa sauti kwa wanawake kwa sababu ya uchumi,” amesema Revocatus Shaba, Mkazi wa Nyegezi jijini Mwanza.
Akiunga mkono hoja hiyo Sheikh wa Wilaya ya Nyamagana, Revocatus Shaba amesema wanaume kukosa unyumba ndani ya ndoa zao zimekuwa ni kesi ambazo wamekuwa wakikutana nazo mara nyingi huku akishauri watu kumrudia Mwenyezimungu.
Akijibu shutma zilizotolewa na wanaume dhidi ya wanawake, Katibu Idara ya Michezo kutoka Jumuiya ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Mwanza, Jackline Daudi amesema,
“Akina mama saizi wako bize sana kutafuta pesa wanaamka saa 11 wanarudi mchana akiwa amechoka mwanaume na mwenyewe anahitaji kwahiyo inakuwa changamoto kwenye suala la ndoa lakini pia wamama wamekuwa ni wababe sana mwanaume anapohitaji na hana pesa inakuwa ngumu mwanamke kumsikiliza mke wake kwa kile anachohitaji”.
Akizungumzia kuhusu ligi hiyo, Katibu wa SMAUJATA kata ya Mkolani, Kabambo Oscar ameeleza kuwa lengo la kuanzisha ligi hiyo ni kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia na kuutokomeza katika jami.
“Tuliona si vyema tukae tu hivihivi tuje na wazo ambalo itakuwa rahisi kuifikia jamii sisi kama SMAUJATA… lakini lengo kubwa la kuanzisha haya mashindano ni kuwaweka vijana pamoja na kutoa elimu juu ya vitendo hivi vya ukatili,” amesema Oscar
ALSO READ | Hizi Ndio Sehemu 10 Zenye Msisimko Mkali Zaidi kwenye Mwili wa Mwanamke