Serikali Yakemea Wakenya Kujihusisha na Kesi ya Tundu Lissu
“Chombo cha kisheria kimepata heshima ya kupata daraja “A” na waangalizi mahususi wa kimataifa. Daraja “A” ndiyo la juu zaidi kwamba chenyewe na nchi yote inafanya vizuri. Tuachane na Propaganda zinazoletwa, na Jana Mhe. Rais amesema, mimi nirudie. Mhe. Rais aliongea kistaarabu, kistaarabu sana na sisi wengine kuna siku nyingine ustaarabu huwa tunauacha nyumbani.
Kwa ndugu zetu Wakenya walikuja wakazuiwa pale Airport, wanasema walikuja kwenye kesi ya Tundu Lissu kusimamia haki za binadamu za Tundu Lissu. Wanasema Mimi ni mwanasheria.
Kwa mujibu wa uelewa wangu wale hawana leseni ya kufanya shughuli ya uwakili Tanzania. Kwahiyo walichokuja kukifanya ni uvunjifu wa sheria zetu, lakini kule kwao yamewashinda. Nyumba yako inawaka moto unataka ukazime kwa jirani? Huo ni unafiki na sisi Watanzania hatutaki Unafiki. Kwenye eneo la haki za binadamu tupo vizuri sana na ninaungana na Mhe. Rais kwa kauli yake jana.”- Dkt. Damas Ndumbaro. Waziri wa Katiba na Sheria.
ALSO READ | Rais Samia Awashukia Wanaharakati wa Kenya: Watovu wa Adabu, Walishavuruga Kwao