Yanga Wala Chuma Moja Simba Ikichukua Ubingwa Ligi ya Muungano Kibabe

Shughuli imemalizika katika dimba la New Amaan Complex, Zanzibar, Mnyama amekata ukame wa kutokushinda mbele ya Wananchi, Young Africans baada ya kuibuka na ushindi wa 1-0 na kutwaa ubingwa wa Kombe la Muungano kwa mara ya saba.

FT: Yanga SC 0-1 Simba SC
⚽ 120+4’ Mwalimu

Yaliojira Kwenye Mchezo Huo:

✍🏼 Kipindi cha kwanza game ilikuwa na matumizi makubwa ya nguvu kwenye mchezo kama huo unahitaji wachezaji wenye utimamu wa mwili ilikushindana .

✍🏼 Simba bila mpira wanazuia na 4-5-1 nafikiri Steve alihitaji kuwa na wachezaji wengi hasa eneo la ndani Kwanini ?

1: Ubora wa Yanga upo kwenye kiungo ( Allan – Pacome – Maxi ) timu ikiwa na mpira wanashambulia eneo la ndani maana yake unahitaji idadi kubwa ya wachezaji ambao watazuia vizuri nafasi eneo la ndani .

2: Simba walifanikiwa kwa plan yao waliwalazimisha Yanga kupitia pembeni zaidi na kukosa ubora eneo la ndani ( ngumu kwasababu wachezaji wao wa mbele wanakuwa mbali na goli ) .

3: Nafikiri Yanga walipata nafasi kubwa kwenye mpira hasa wakati wanaanza build up ni kwasababu Simba hawaweki presha kuanzia juu , maana yake Yanga wanapata muda na nafasi kwenye mpira tatizo ni wakivuka mstari wa kati wanakosa machaguo ya pasi zao kupitia ndani .

✍🏼 Kipindi cha pili ni kama timu zote ziliamua kufunguka Simba wakatoka kwenye low block viungo wa Yanga space zikawa zinapatikana kwenye half spaces tatizo likawa ni maamuzi yao ya mwisho wakiwa na mpira .

✍🏼 Nafikiri kocha wa Simba “ Stave Berker “ alihitaji umiliki zaidi ya mpira utamfanikisha kuifungua Yanga lakini kitu kimoja cha msingi zaidi wakiwa na mpira wanakosa runners eneo la mbele wachezaji wengi wanahitaji mpira mguuni ngumu kupata nafasi eneo la mbele .

NOTE :

1: Chama anarahisisha sana wakati timu inashambulia .

2: Kassali amefanya saves nzuri sana kuibakisha Simba mchezoni .

3: Back line za timu zote zimecheza game bora ( Shida mipambano yao vizuri ) .

4: Loemba amebadilisha game kWa Simba hasa wakiwa na mali .

5: Mwalimu utulivu mkubwa kwenye Penalti 🤝

FT : Yanga 0-1 Simba

Uchambuzi by : @kelvinrabson_

Related Posts