Azam FC Yatozwa Milioni 5 Kwa Kuingia Uwanjani Kwa Mlango Usio Rasmi

Klabu ya Azam imetozwa faini ya Tsh. milioni tano kwa kosa la viongozi wa benchi la ufundi pamoja na wachezaji kutumia mlango usio rasmi kuingia uwanjani kinyume na matakwa ya kanuni za Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo na makubaliano yaliyofanyika kwenye kikao cha maandalizi ya mchezo wa Dabi ya Mzizima.

Adhabu hiyo imetolewa leo Aprili 20, 2026 na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kufuatia kikao chake cha Aprili 18, 2026 ambapo tukio hilo lilitokea kwenye mchezo kati ya Azam FC dhidi ya Simba SC uliomalizika kwa sare tasa katika dimba la Azam Complex, Chamazi.

Related Posts