Ali Kamwe Afunguka Sababu ya Yanga Kumfuta Kazi Kocha Pedro Goncalves

Ali Kamwe Afunguka Sababu ya Yanga Kumfuta Kazi Kocha Pedro Goncalves
Ali Kamwe Afunguka Sababu ya Yanga Kumfuta Kazi Kocha Pedro Goncalves

Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe, amesema sababu kubwa ya uongozi wa klabu hiyo kuachana na Kocha, Pedro Goncalves ni mwenendo usioridhisha wa timu licha ya kuendelea kushinda mechi na kuongoza ligi.

Akizungumza katika mahojiano Mei 7, 2026 Kamwe alisema viongozi wa Yanga waliona dalili za matatizo mapema kupitia kiwango cha timu uwanjani.

“Hatupo tayari timu ipoteze mchezo halafu ndio tuseme tumegundua shida, viongozi wazuri huwa wana uwezo wa kuangalia tatizo linaanzia wapi.”

Kocha, Pedro Goncalves
Kamwe alieleza kuwa kiwango cha jumla cha timu kilikuwa hakiridhishi na kilitoa viashiria kuwa huenda timu ingeanza kupoteza alama katika michezo ijayo.

“Performance ya timu kwa ujumla bado hairidhishi, performance inakupa viashiria kuwa muda si mrefu tungeweza kudondosha alama.”

Kauli hiyo imezua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki wa soka nchini, hasa ikizingatiwa kuwa Yanga bado ipo kileleni mwa ligi kuu huku ikiendelea kufanya vizuri kwenye matokeo.

Related Posts