Mastaa Wampongeza Jackie Cliff Baada ya Kushare Picha za Ujauzito

Jackline Patrick maarufu kama Jack Patrick au Jackie Cliff (@mscliff_) ameendelea kuteka mijadala kwenye mitandao ya kijamii baada ya kushiriki picha mpya zikimuonyesha akiwa na ujauzito.

Picha alizoweka kupitia akaunti yake ya Instagram zimepokelewa kwa hisia tofauti huku mastaa mbalimbali, mashabiki pamoja na watu maarufu wakimiminika kwenye ukurasa wake wakimtumia salamu za pongezi na kumtakia kila la heri katika hatua hiyo mpya ya maisha yake.

 

Jackline, ambaye aliwahi kuwa kwenye uhusiano na msanii maarufu wa RnB kutoka Tanzania, Juma Jux ameonekana mwenye furaha kubwa kwenye picha hizo jambo lililozidi kuwavutia mashabiki wake wengi mtandaoni.

Baadhi ya watu maarufu na followers wake wameendelea kumuombea afya njema yeye pamoja na mtoto anayemtarajia, huku wengine wakieleza kufurahishwa na hatua hiyo mpya ya maisha yake.

Mpaka sasa, picha hizo zimeendelea kusambaa kwa kasi kwenye majukwaa mbalimbali ya mitandao ya kijamii na kuibua gumzo kubwa miongoni mwa watumiaji wa mtandao.

Related Posts