Mbwana Samatta Aachana Rasmi na Taifa Stars Baada ya Miaka 15

Mbwana Samatta Aachana Rasmi na Taifa Stars Baada ya Miaka 15

Nahodha na mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Mbwana Samatta, ametangaza rasmi kustaafu kuichezea timu hiyo baada ya kuitumikia kwa takribani miaka 15.

Samatta ametoa taarifa hiyo usiku wa kuamkia leo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, ambapo amewashukuru Watanzania na kueleza kuwa ulikuwa wakati wa fahari kubwa kwenye maisha yake ya soka.

Kutoa Nafasi kwa Vipaji Vipya

Katika ujumbe wake, nahodha huyo wa zamani wa KRC Genk na Aston Villa amebainisha kuwa umefika wakati sahihi wa kupisha damu changa na vipaji vipya ili kuivusha Taifa Stars hatua inayofuata.

Related Posts