Moto Mkubwa Waibuka Hifadhi ya Kilimanjaro, Uchunguzi Waanza

Moto Mkubwa Waibuka Hifadhi ya Kilimanjaro, Uchunguzi Waanza
Moto Mkubwa Waibuka Hifadhi ya Kilimanjaro, Uchunguzi Waanza

Moto Mkubwa Waibuka Hifadhi ya Kilimanjaro, Uchunguzi Waanza

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limetangaza kuibuka kwa moto katika eneo la Kikerelwa, ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro, maeneo yanayopakana na Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa TANAPA, moto huo umeibuka leo, Septemba 3, 2026, majira ya saa 9:30 alasiri, huku juhudi za kuudhibiti zikiendelea.

TANAPA imepeleka timu ya uzimaji moto ya Jeshi la Uhifadhi kwa kushirikiana na wadau wa uhifadhi na utalii pamoja na wananchi wa vijiji vya jirani, katika jitihada za kuuzima moto huo.

Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana, huku uchunguzi ukiendelea kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama.

TANAPA imesema kuwa shughuli za utalii katika Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro zinaendelea kama kawaida, na kuwahakikishia watalii, wananchi pamoja na wadau kwamba usalama wa hifadhi na watalii unaendelea kupewa kipaumbele.

Related Posts