Chauma Kumenoga Huko, Maandalizi ya Mapokezi ya Wanachama Wapya Yaandaliwa
Edward Kinabo, mwanachama wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) amesema maandalizi kwa ajili ya mapokezi ya wanachama wa chama hicho yatakayofanyika Ukumbi wa Ubungo Plaza mkoani Dar es Salaam siku ya kesho Jumatano yanaendelea vyema.
Akizungumza na wanahabari siku ya Jumanne, Kinabo amesema wanategemea kuwa na watu zaidi ya 3000 kwa ajili ya kushiriki hafla hiyo ya mapokezi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mapokezi hayo, Catherine Ruge ameeleza kuwa idadi hiyo kubwa ya watu hao inayotarajiwa kupokelewa rasmi ndani ya chama hicho inatoka mikoa mbalimbali nchini.