Donald Trump Anaweza Kumsamehe P Diddy Haki Isipotendeka
Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema yuko tayari “kuangalia ukweli” na kufikiria kumsamehe msanii Sean “Diddy” Combs, endapo atapatikana na hatia kwenye kesi yake inayoendelea.
Akizungumza na waandishi wa habari Ikulu ya White House, Trump alisema: “Kama si haki, nitaiangalia. Sijafuatilia kwa karibu, lakini nataka iwe hukumu ya haki.”
Diddy, mwenye umri wa miaka 55, anakabiliwa na mashtaka mazito mahakamani Manhattan, yakiwemo usafirishaji haramu wa watu kwa ajili ya ngono, kupanga njama ya kihalifu, na kuendesha biashara ya ukahaba. Amekana mashtaka yote. Ushahidi uliotolewa na msaidizi wake wa zamani umechochea gumzo zaidi, ukidai kuwepo kwa miaka ya unyanyasaji.
Trump alikiri kuwa aliwahi kuwa na urafiki wa karibu na Diddy, ingawa urafiki huo ulivunjika baada ya yeye kuingia kwenye siasa. Ingawa bado hakuna ombi rasmi la msamaha lililowasilishwa, Trump alidokeza kuwa “watu wanafikiria kuhusu hilo.”
Kesi bado inaendelea, na iwapo Trump ataingilia kati kutegemea uamuzi wa mahakama na kama ombi rasmi litatolewa.