Ile Fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) kati ya Yanga dhidi ya Singida Black Stars, wakati wowote inaweza kurejea Zanzibar, huku tarehe ikiwa bado haijajulikana.
Ikumbukwe kuwa, fainali iliyopita kati ya Azam dhidi ya Yanga ilichezwa kwenye uwanja huo na Yanga kutetea taji kwa mara ya tatu mfululizo kwa penalti.
Taarifa kutoka ndani ya TFF ni kwamba, mchakato huo ulikumbana na machaguo mawili pekee ya wapi mechi hiyo ikapigwe. Viwanja vilivyo pendekezwa vilikuwa CCM Kirumba, Mwanza na New Amaan Complex, Zanzibar.
Hata hivyo, arena tunafahamu, Uwanja wa Kirumba haukuwaridhisha maofisa waliokwenda kuukagua, hali iliyosababisha chaguo libaki kwa Amaan pekee.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, mabosi wa CRDB ambao ndio wadhamini wa mashindano hayo nao walikuwa na mapendekezo ya fainali hiyo kurudishwa Zanzibar.
