ALIYEKUWA Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi ni miongoni mwa makocha wanaotajwa kukifundisha kikosi cha APR ya Rwanda 🇷🇼 msimu ujao, baada ya mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Rwanda kuachana na Mserbia Darko Novic.
.
Gamondi aliyeifundisha Yanga kwa mafanikio, kwa sasa yupo huru baada ya kuachana na Al Nasr ya Libya, ingawa taarifa kutoka Rwanda zinaeleza ni miongoni mwa wanaofuatiliwa kutokana na uwezo alionao.
.
Mbali na Gamondi, makocha wengine ni Miguel Cardoso anayeifundisha Mamelodi Sundowns kwa sasa pamoja na na Nabil Maaloul aliyekuwa USM Alger. APR itakayoshiri- ki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao, imechukua ubingwa wa Ligi Kuu Rwanda ikiwa na pointi 67.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *