Dkt. Samwel John Marwa, daktari na mwanachama halali wa Young Africans SC mwenye kadi namba TZIRI03003030 alifungua maombi chini ya hati ya dharura akiomba kibali cha kufungua shauri la mapitio ya Kimahakama (Judicial Review) dhidi ya uamuzi wa Bodi ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (TPLB) wa kuahirisha mechi ya ligi (mechi Na. 184) kati ya Young Africans SC dhidi ya Simba SC ambayo ilipangwa kuchezwa tarehe 08 Machi 2025
Katika hoja zake alikuwa anaomba Mahakama kutoa amri Certiorari ya kufuta uamuzi wa TPLB wa kuahirisha mechi hiyo, amri ya Mandamus ya kuilazimisha TFF (Shirikisho la Soka Nchini) na TPLB kuipa Young Africans SC pointi 3 na mabao 3 kwa mujibu wa sheria, na ulipwa gharama za shauri hili, na pia amri nyingine yoyote itakayoonekana haki na stahiki
Wakili wa wajibu maombi Rahimu Shabani alipinga uhalali wa shauri hilo kwa hoja mbili;
Kwanza, shauri hilo limeletwa Mahakamani kabla ya wakati, na Mhakama haina mamlaka (jurisdiction) ya kusikiliza shauri hilo, kufuatia hilo Mahakama ilisikiliza hoja ya pili tu kuhusu mamlaka, kwa sababu hoja ya kwanza haikuwasilishwa kwa kina
Wajibu maombi walisema, Katiba ya TFF na kanuni za ligi 2024 zinakataza mtu yeyote kufungua kesi ya masuala ya ligi katika Mahakama ya kawaida, kifungu cha 25(4) cha kanuni za ligi kinakataza kupeleka migogoro ya ligi Mahakamani, na kifungu cha 66 na 67 cha Katiba ya TFF kinatamka kuwa migogoro yote ya mpira itamalizwa ndani ya mfumo wa TFF, na hatimaye katika CAS (Court of Arbitration for Sport) baada ya njia zote za ndani ya TFF kuisha
Hapa pia imeelezwa kwamba, FIFA pia inapiga marufuku kufungua mashauri ya mpira kwenye Mahakama za kiraia isipokuwa kwa idhini ya taasisi za kimataifa
Kwa upande wake, Wakili wa muombaji, Bw. Jesse, alidai kuwa shauri hilo halihusu migogoro ya ndani ya TFF bali ni dhidi ya TFF, muombaji si mwanachama wa TFF hivyo hajazuiliwa na Katiba yao, na kwamba ana haki ya kuomba suluhu Mahakamani kwa kuwa hakuna chombo rasmi cha kutatua mzozo kama huo kwa watu wa nje
Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, Jaji alifanya uchambuzi na kusema yafuatayo.