Majina ya Mastaa Waliotajwa Kwenye Kesi ya P Diddy
Kesi ya Sean “Diddy” Combs kuhusu madai ya usafirishaji wa watu kwa ajili ya ngono imeendelea kuvuta hisia nyingi tangu ianze Mei 5 huko Manhattan, New York. Mastaa kadhaa maarufu wametajwa kwenye kesi hiyo ingawa hawahusishwi moja kwa moja na makosa yoyote.
Kanye West, Michael B. Jordan, Kid Cudi, Mike Myers, Michelle Williams, na Prince ni miongoni mwa majina yaliyotajwa wakati wa uchaguzi wa majaji. Kanye alitajwa kutokana na ukaribu wake na Diddy, huku Michael B. Jordan akihusishwa na uhusiano wake wa zamani na Cassie Ventura, aliyekuwa mpenzi wa Diddy.
Cassie, ambaye alitoa ushahidi mahakamani, alieleza mateso aliyoyapata kutoka kwa Diddy wakati wa uhusiano wao, akidai alilazimishwa kushiriki kwenye “Freak-Offs” — sherehe za ngono na madawa ya kulevya zilizoendelea hadi kwa siku nne.
Majina mengine yaliyotajwa ni pamoja na Drake, French Montana, Britney Spears, Bruce Willis na Eddie Murphy, wakihusishwa na matukio tofauti katika maisha ya Cassie na Diddy.
Kesi hii inaendelea kushika vichwa vya habari, huku ushahidi zaidi ukitarajiwa kufichuliwa.