Habari za majonzi zimeendelea kuitikisa familia ya marehemu msanii Hawa Hussen maarufu kama Carina, baada ya mama yake mzazi, Fatma Maruzuku, kufariki dunia.

Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa mama Carina amefariki dunia yapata siku arobaini tu tangu mwanawe azikwe.

Kulingana na taarifa zilizothibitishwa na mmoja wa wanafamilia aliyezungumza na Global TV, marehemu mama Carina alikuwa akiumwa kwa muda mrefu akisumbuliwa na maradhi ya kisukari na shinikizo la damu (presha).

Hali yake ya afya haikuwa nzuri kiasi kwamba hakuhudhuria hafla ya kumbukumbu ya siku arobaini ya mwanawe iliyofanyika wiki iliyopita.

Kifo hiki kimetikisa wengi hasa ukizingatia kuwa familia ilikuwa bado katika kipindi cha maombolezo ya msanii huyo aliyekuwa maarufu kwa sauti yake ya kuvutia na mchango wake katika tasnia ya muziki.

Wengi mitandaoni wameeleza masikitiko yao, wakituma salamu za pole kwa familia iliyogubikwa na huzuni mara mbili kwa kipindi kifupi.

Tunatoa pole kwa familia, jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu mzito.

Roho ya marehemu Fatma Maruzuku ipumzike kwa amani, pamoja na binti yake Carina walioungana tena milele.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *