NyokaNyoka

Mamlaka nchini India imemkamata mwanamume mmoja kwa kujaribu kuingiza nyoka wenye simu ambao ni adimu kupatikana na wanyama wengine, nchini humo.

Raia huyo wa India, ambaye alikuwa akirejea kutoka Thailand, alizuiwa na maafisa wa forodha katika uwanja wa ndege mjini Mumbai siku ya Jumapili.

Maafisa walisema nyoka hao 47 wenye sumu kali, walipatikana wamefichwa kwenye begi la mwanamume huyo.

Wanyama hao wamechukuliwa chini ya sheria mbalimbali za ulinzi wa wanyamapori nchini India.

Mwanamume huyo hakutajwa jina lake na yuko chini ya ulinzi. Hajazungumzia lolote tangu akamatwe.

Maafisa wa forodha waliweka picha kwenye mtandao wa X za nyoka wa rangi mbalimbali wakitambaa kwenye sahani.

Katika ujumbe wao, walisema wamekamata nyoka watatu wenye pembe mfano wa buibui, kasa watano wa Asia na nyoka 44 wa Indonesia kutoka kwa abiria huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *