Mwanamuziki D Voice Athibitisha Zuchu Bado Yupo WCB

Licha ya drama zinazoendelea leo kuhusu Zuchu kufuta utambulisho wa WCB Wasafi kwenye Instagram, lebo hiyo imeonyesha bado ina mahusiano ya karibu na msanii huyo. Kupitia ukurasa rasmi wa WCB, wamepost video ya Zuchu akishiriki kwenye challenge ya wimbo mpya wa Barnaba “Salama”, aliomshirikisha Diamond Platnumz hatua inayoashiria kuwa bado wanampa nafasi ya kuonekana kupitia kazi za lebo, hata zisizomuhusu.

Zaidi ya hapo, msanii mwenzake wa WCB, D Voice, ametangaza ujio wa wimbo wake mpya “Baby Mpya” akimshirikisha Zuchu, hatua inayozidi kuonesha kuwa Zuchu bado ni sehemu ya familia ya Wasafi, licha ya ishara za sintofahamu kwenye mitandao ya kijamii.

Ingawa hatua ya Zuchu kuondoa bio ya WCB kwenye Instagram imezua maswali kuhusu hatma yake ndani ya lebo hiyo, ushiriki wake kwenye miradi rasmi ya WCB unaonyesha bado yupo ndani ya mfumo. Hali hii inaweza kuwa sehemu ya mabadiliko ya kimkakati au masuala ya muda mfupi ya kihisia. Drama inaendelea, lakini kwa sasa Zuchu bado yupo sana WCB.

ALSO READ | Zuchu Ajiondoa WCB?, Afuta Utambulisho Wake IG na Kuzua Maswali

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *