Meneja wa mwanamuziki @mavokali_ , Jembe One ameweka wazi hali ya kiafya ya msanii wake kwa kusema alipatwa na tatizo la afya ya akili ingawa kwa sasa anaendelea vizuri.

Jembe ameiambia Mwananchi kuwa msanii wake alipata tatizo hilo baada ya kutapeliwa na kampuni moja ya Uingereza inayofanya kazi ya usambazaji muziki ambayo hakutaka kuitaja jina.

Huku akiahidiwa kufanya kolabo na wasanii kama Shakira, Maluma na.Beyonce. “Hali yake kwa sasa anaendelea vizuri. Sio vibaya sana tunaendelea kupambana naye ili aweze kukaa sawa, akiwa peke yake ndio anakuwa na mawazo sana. Kwa hiyo madaktari wamemsaidia kwa kiasi chake ili aweze kuwa sawa, kwa sababu alikuwa anapenda kukaa peke yake.”

Meneja huyo amesema Mavokali aliingia mkataba na kampuni
inayojihusisha na kusambaza kazi za wasani nchi tofauti tofauti,
huku wakimuahidi kufanya kolabo na mastaa mbalimbali bila
mafanikio. “Kampuni hiyo ilimuahidi remix ya wimbo wa ‘Mapopo’ kwa sababu tumeshafanya na Rayvanny, tukategemea kupata International Artist. Walikuja na njia ya kwamba wanataka kumpa msanii ambaye atafanya naye remix.
“Wakaja na majina ya wasanii baada ya hilo tukaona ni kitu kizuri tufanye nao kazi.

Changamoto ni kwamba wasanii ambao
waliwataja wakashindwa kuwafikia. Wakaja na wasanii wengine
ambao kwenye mkataba hawapo kwahiyo tulipoanza kuhoji ndio
changamoto ilipoanza,” amesema.

Amesema baada ya kutokuwa na maelewano. Kampuni hiyo
ilichukua hatua ya kuzifungia akaunti zote za msanii huyo.
“Hiyo ishu imekaa kisheria zaidi. Msaada ambao tunautegemea ni.wakisheria. Wanasheria ndiyo wanapambana ili hii ishu iweze
kuisha, kwa sababu siyo ishu ya jana au juzi ni ishu ambayo inafika.mwaka wa pili sasa.Vitu vinazidi kuwa viqumu. Wale watu wamezuia hela zetu tumeamua kuongea ili jamii iweze kuelewa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *