Rais Ruto Vs Rigathi GachaguaRais Ruto Vs Rigathi Gachagua

Rais Ruto Amlipua Rigathi Gachagua na Chama Chake Kipya

Rais wa Kenya, William Ruto, ameendeleza mashambulizi yake dhidi ya aliyekuwa Naibu wake, Rigathi Gachagua, akimtuhumu kwa kuendeleza siasa za matusi na ukabila badala ya kuzingatia maendeleo ya wananchi.

Akizungumza Ijumaa, wakati wa ukaguzi wa mradi mkubwa wa umwagiliaji wa Galana Kulalu katika Kaunti ya Tana River, Rais Ruto alieleza kuwa viongozi hawatapata kura kwa matusi, bali kwa kazi wanazofanya.

“Hakuna mtu atapata kura ati kwa sababu alikuwa na matusi mingi. Mtu atapatiwa kura kwa sababu kuna kazi amefanya na inaonekana na wananchi,” alisema.

Alisema wakati huu si wa siasa bali ni wa maendeleo, akiwasihi viongozi kuepuka siasa za chuki, ukabila na ushabiki wa vyama.

“Sio wakati wa siasa…sio wakati wa marengo, kabila, dini sijui chama…wakati huu ni wa sote kuungana na kushughulikia mambo ya muhimu yatakayobadilisha maisha ya Wakenya,” aliongeza.

Kauli hizo ziliungwa mkono na Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki aliyekuwa akihutubia wakazi wa Kaunti za Murang’a na Meru, ambapo alitoa onyo kwa wanaoanza kampeni mapema kupitia chama kipya.

“Wale wanaomba viti wajue hakuna uchaguzi sasa. Wangojee siku ya uchaguzi, ndipo tutanyoroshana,” alisema Kindiki.

ALSO READ | Mbasha Amchana Aliyekuwa Mkewe, Flora baada ya Kubadili Jina na Kutangaza Uongozi Mpya

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *