Roma MkatolikiRoma Mkatoliki

Kupitia maoni yake, Roma ameashiria kuwa msanii atakayethubutu kuachia wimbo wiki hii lazima awe na mkakati madhubuti wa kuvutia umakini wa watu. Kwa mtazamo wake, kasi ya matukio yanayovuma sasa inahitaji msanii kuwa amejipanga vilivyo ili kazi yake isizame kwenye bahari ya drama na headlines nyingine.

Kauli hii inakuja wakati ambapo gumzo la ndoa ya Diamond Platnumz na Zuchu, ujauzito wa Lulu na pete za ndoa za Nandy zilizopotea sambamba na mijadala ya kisiasa inayoendelea nchini, limegeuza taswira ya mazungumzo kwenye mitandao ya kijamii. Roma anaonekana kuonya kwa hekima kwamba huu sio wakati sahihi kwa msanii kiacha kazi mpya ya sanaa —hasa wakati “attention” ya watu ipo sehemu nyingine.

Hii ni tahadhari muhimu kwa wasanii wanaotafuta nafasi ya kung’aa kwenye soko la muziki wamba kuachia kazi mpya sio tu kuhusu ubora wa wimbo, bali pia muda na mazingira ya kuachiwa wimbo huo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *