Mechi ya Kirafiki ambayo imepigwa KMC COMPLEX kati ya Yanga SC dhidi ya Singida Black Stars imeisha kwa Singida BS kushinda mabao 3-2.
Mabao ya Yanga SC yamefungwa na Prince Dube na Denis Nkane wakati mabao ya Singida Black Stars yamefungwa na Arthur Bada, Jonathan Sowah na Elvis Rupia.
Singida Black Stars imejipima nguvu kujiandaa na mechi zake mbili dhidi ya Simba SC, Mei 28 na Mei 31.
FT. Yanga SC 2-3 Singida Black Stars.