Yanga Yaondoka Botswana na Sare, Mwalimu Aokoa Jahazi Dakika za Mwisho

Yanga Yaondoka Botswana na Sare, Mwalimu Aokoa Jahazi Dakika za Mwisho
Yanga Yaondoka Botswana na Sare, Mwalimu Aokoa Jahazi Dakika za Mwisho

Yanga Yaondoka Botswana na Sare, Mwalimu Aokoa Jahazi Dakika za Mwisho

Klabu ya Yanga SC imeanza kampeni yake ya msimu mpya wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) kwa matokeo ya sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Gaborone United ya Botswana.

Mchezo huo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya awali uliopigwa katika Uwanja wa Taifa wa Gaborone, ulioshuhudia wenyeji wakitawala sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza na kupata bao la uongoza kupitia kwa mshambuliaji Obry Amseb mnamo dakika ya 33.

Pamoja na Yanga kuongeza shinikizo kusaka bao la kusawazisha, safu ya ulinzi ya Gaborone United iliendelea kuwa imara hadi kipindi cha pili kikielekea ukingoni. Hata hivyo, jitihada za Yanga zililipa katika dakika za nyongeza (90+5′) wakati Mwalimu alipofunga bao la kusawazisha na kuokoa jahazi la miamba hiyo ya Tanzania.

Matokeo hayo yanaipa Yanga faida kubwa ya bao la ugenini kuelekea mchezo wa mkondo wa pili utakaopigwa jijini Dar es Salaam, ambapo watakuwa na fursa ya kutumia uwanja wa nyumbani kusaka tiketi ya kutinga hatua inayofuata.

ALSO READDudu Baya Amponza Afande Sele! Apewa Onyo kali na Serikali Kutetea Makosa haya, Waziri Katambi Awaka

Related Posts

One thought on “Yanga Yaondoka Botswana na Sare, Mwalimu Aokoa Jahazi Dakika za Mwisho

Comments are closed.