Auawa na Wanamchi Wenye Hasira Kali Baada ya Kuitiwa Mwizi na Mpenzi wake

Auawa na Wanamchi Wenye Hasira Kali Baada ya Kuitiwa Mwizi na Mpenzi wake
Auawa na Wanamchi Wenye Hasira Kali Baada ya Kuitiwa Mwizi na Mpenzi wake

Tafadhali Zingatia: Ikiwa unasoma kwenye PHOENIX, tafadhali bofya kitufe cha “Soma Makala Asili” kilicho upande wa juu kulia ili kusoma makala kamili.

Kijana mwenye umri wa miaka 24 kutoka Kenya, Amos Manasseh, amefariki dunia baada ya kushambuliwa na wananchi wenye hasira katika Kaunti ya Nyamira wakimtuhumu kuwa mwizi.

Kwa mujibu wa taarifa zinazosambaa, Amos alikuwa na mgogoro wa kimapenzi na mpenzi wake baada ya kudai kuwa amemsaliti.

Inadaiwa alifika nyumbani kwa mwanamke huyo ili kuchukua mtungi wa gesi aliokuwa amemnunulia awali kama zawadi.

Hata hivyo, mwanamke huyo alidai kuwa Amos alikuwa akiiba na kuanza kupiga kelele kuomba msaada. Wananchi waliokusanyika eneo hilo walimshambulia Amos kwa kipigo na mawe bila kusubiri uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo.

Amos alifariki kutokana na majeraha aliyoyapata katika shambulio hilo.

Related Posts